Serikali imewaomba radhi walemavu na Watanzania wote kutokana na nguvu kubwa iliyotumika kwa walemavu waendesha bajaji wa Jiji la Dar es Salaam waliokuwa wakitaka kwenda kumuona Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ameomba radhi leo (Jumanne) na kukiri kuwa pamoja na walemavu hao kuwa na makossa, lakini nguvu ya polisi ilipitiliza na akasema wameshawasilina na mkoa husika kupitia ustawi wa jamii.

Waziri alikuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu, Stella Ikupa ambaye alitaka kujua namna gani Serikali inavyoweza kuliona jambo hilo lililosababisha walemavu kupigwa, kuburuzwa chini na kudhalilishwa kwa kiasi kikubwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com