Msanii mpya kutoka WCB, Lava Lava, amefunguka mambo mengi kuhusu muziki wake pamoja na kueleza jinsi anavyomkubali muimbaji Alikiba ambaye ni mpinzani mkubwa wa bosi wake, Diamond Platnumz.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake mpya ya wimbo, Tuachane, amedai amekuwa akiufutilia muziki wa Alikiba kwa muda mrefu.

“Alikiba ni msanii mzuri sana, nampenda sana,” alisema Lava Lava. “Ni mkongwe kwenye muziki, miaka yote namuangalia na kujifunza vingi kutoka kwake”

Pia muimbaji hayo amedai haioni kama kuna bifu kati ya bosi yake na Alikiba ila anachokiona ni ushindani kati ya wawili hao.

“Mimi naona baada ya ushindani kuanzishwa na muziki wetu umefika mbali, kwa hiyo kushindanishwa kwao mimi naona ni sawa kwa sababu muziki unafika mbali na watu wanakuwa na speed ya kazi lakini siyo kwa ubaya,” alisema Lava Lava.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amedai alikaa kipindi cha mwaka mmoja WCB bila kuona na Diamond.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com