Klabu ya Manchester United imeonyesha imepania kumbakiza kipa wake David De Gea baada ya kukataa kumuuza kwa Real Madrid.

Man United imekataa kitita cha pauni milioni 60 ambayo ingekuwa rekodi ya usajili kwa kipa kutoka katika klabu ya England.

Ingawa hali hiyo imeonyesha kuwashangaza wengi, inawezekana Real Madrid wakarejea na kitita kikubwa zaidi ili kumnasa De Gea ambaye ni raia wa Hispania.

De Gea alitokea katika jiji la Madrid akiwa na Atletico Madrid na kujiunga na Manchester United akiwa kipa kinda.


Lakini kwa misimu miwili mfululizo, amekuwa tegemeo kuu la kikosi cha Man United ambacho kimekuwa kikiyumba.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com