Usikilizwaji kesi ya dawa ya kulevya inayomkabili Miss Tanzania Wema Sepetu wapigwa kalenda.

Usikilizwaji wa kesi ya dawa za kulevya inayomkabili aliyekuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu uliokuwa uanze leo, umesogezwa hadi Julai 10 mwaka huu sababu Hakimu anayesikiliza kesi hiyo yuko likizo.

Wema ambaye pia ni msanii wa filamu nchini, anashtakiwa na wafanyakazi wake wawili, Angelina Msigwa (21) pamoja na mkulima Matrida Abas (16) ambao wote kwa pamoja wanawakilishwa na Wakili Peter Kibatala.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kuwa kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa lakini Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba anayesikiliza kesi hiyo yupo likizo.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mwambapa ameaihirisha kesi hiyo hadi Julai 10 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kuja kusikilizwa.

Inadaiwa kuwa, Februari 4, mwaka huu huko nyumbani kwao Kunduchi Ununio jijini Dar es Salaam Watuhumiwa hao wote walikutwa wakiwa na msokoto mmoja pamoja na vipisi viwili vya bangi vyenye gramu 1.80 ambavyo ni dawa za kulevya.

Washitakiwa wote wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kila mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao walisaini bondi ya milioni tano.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com