Mwimbaji staa wa Bongofleva Harmonize kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM amefunguka na kudai kuwa mipango yake ni kufanya kazi label kubwa kama Young Money au Roc Nation endapo ataondoka WCB.

Harmonize amesema WCB ni moja ya label zinazofanya vizuri Afrika hivyo hawezi kutoka kwenye label hiyo na kwenda kwenye label nyingine ndani ya Afrika badala yake atakwenda kimataifa zaidi ingawa kwa sasa ana malengo ya kuifanya WCB iwe kubwa.

“Lengo langu ni kuifanya WCB iwe kubwa, ifike mbali panapo majaaliwa ya Mwenyezi Mungu na support ya watanzania lakini ikitokea kufanya kazi na Label nyingine na wish label yoyote tunayoweza kufanya kazi vizuri kama Roc Nation au Young Money. Siwezi kutoka WCB nikaenda label nyingine. Ukizungumzia WCB ni label kubwa Afrika. kwa hiyo, nikitoka Afrika may be Roc Nation au Young Money.” – Harmonize

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com