Mpenzi mpya wa Harmonize

Baada ya kuachana na mrembo wa filamu Tanzania Jacqueline Wolper, muimbaji wa  wimbo  Happy BirthDay kutoka WCB, Harmonize, ameonesha picha ya mpenzi wake mpya mzungu pamoja na kuthibitisha ni mjamzito.

Muimbaji huyo ambaye alikuwa kimya kuzungumzia mahusiano yake mapya na mzungu huyo licha ya kuzungumzwa na watu kwenye mitandao ya kijamii, Jumapili hii ameonyesha vipimo vya Ultrasound vikionesha mpenzi wake huyo mzungu ni mjamzito.

“Mnh! nawaza huu mchanganyiko wa damu ya kimakonde na ya kizungu sijui itatuletea mwana gani… asa nikiona kakomwe hapo, kananistua😁…Chonde mtoto chukua vyote kwangu ila kwenye rangi jitahidi uibe ya mama yako…..!!! nikavimbe Mtwara 😊,” aliandika Harmonize Instagram.

Hata hivyo muimbaji huyo hakuweka wazi ujauzito huo ni wa miezi mingapi.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com