Msanii wa Bongo Fleva kutoka kundi la Weusi, G Nako ameelezea issue yake ya kulala kwenye jeneza kama inavyoonekana kwenye video ya wimbo ‘Lucky Me’.


G Nako amesema baada ya video hiyo kutoka kuna watu wameogopa na kuwa na hofu lakini baada ya kuwaelewesha walielewa.
“Sijavuka mipaka nilichokuwa najaribu kukifanya ni sanaa, na sanaa haina mipaka na kuna baadhi ya watu wamepokea vizuri asilimia ndogo wamepokea kidogo lakini wakieleweshwa wanaelewa,” ameiambia E-Newz ya EATV.

“Watu wanaingia kwenye majeneza kila siku, watu wanauliwa kwenye movie kila siku, sio kitu kigeni sana ni kwa sababu tumechelewa kuingia kwenye tasnia ya muziki. Jeneza lilikodishwa, kununua kidogo itakuwa ngumu, actually walikuwepo wenye mali yao kwa hiyo baada ya kumaliza kulitumia wakalichukua kwenda kufanyia shughuli nyingine,” ameongeza G Nako.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com