Mwimbaji staa wa Bongofleva kutoka WCB Diamond Platnumz amefunguka kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM na kusema kuwa sifa ya kwanza ya WCB ni kumtoa msanii kwenye hali ngumu ili waweze kufanikiwa wote kwa kuwa huwa na adabu na kujituma.

Diamond amesema kuwa wengi wanaotoka katika familia a kitajiri wanakuwa hawana adabu kwa kuwa wanajua kwao kuna hela hivyo hawawezi kujituma ndiyo sababu WCB huchukua watu kutoka familia za chini ili wawashike mkono na wao waweze kusaidia ndugu zao.

“Kweli sifa ya kwanza WCB ni kutoa msanii ambaye ametoka kwenye familia ya chini – kwenye hali ngumu na maisha magumu kwa sababu sisi tunajitahidi kujiajiri wenyewe kwa wenyewe kutengeneza riziki japo muziki wetu haujawahi kuwa na riziki. Hivyo at list kidogo hiki tule wote.

“Kwa sababu tunaamini watu kutoka mtaani wanakuwa na vipaji vya kweli. Wanakuwa na njaa ya kujituma, wanakuwa na nidhamu na wanaogopa wasije kurudi tena katika mtaa lakini watoto wa kitajiri wanakuwa hawana nidhamu kwa kuwa wanajua kwao wana hela. Kwa hiyo, yeye haogopi kufanya kazi kwa bidii anajua hata asipofanya hivyo baba yake ana hela, akifa atarithi mali zake zote.

“Kwa hiyo, sisi tunaamini sana kwamba, wale wameshafanikiwa. Ni mara kumi sisi tukatumia nafasi hii kusaidia ndugu zetu wa mtaani kwa sababu wapo wengi wanaohitaji sisi tuwashike mkono nao wafike sehemu fulani. Kesho na kesho kutwa waje kuwasaidia ndugu zao.” – Diamond

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com