Msanii wa Bongo Fleva, Chege amedai  akitaka kwenda studio kurekodi ni lazima aende na  watu zaidi ya watano.

Muimbaji huyo amekiambia Kipindi cha XXL cha Clouds FM  kuwa huo umekuwa ni mtindo wake tangu akiwa TMK Family ambapo walikuwa wanaenda studio  kama kundi.

“Mimi siwezi kwenda studio pekee yangu, siamini kwenda studio pekee yangu lazima niende na watu ambao tutasaidiana nao, aidha watanipa maneno. Naamini unapoenda studio na watu zaidi ya watano au sita ndio unaweza ukafanya kitu kizuri kwa sababu hata katika kuongea unaweza kukosea point na akakurekebisha lakini asingekuwepo unaona ni pont sahihi,” amesema Chege

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com