Msanii Ben Pol ameonyesha kuchoshwa na vitendo vya watu kwenye mitandao ya kijamii hasa wale ambao kazi yao ni kutukana watu na kuwaponda wengine kwenye mitandao hiyo na kusema hakuna mtu amewahi kupata tuzo kwa kutumia mitandao ya kijamii vibaya.

Ben Pol ambaye siku kadhaa zilizopita amekuwa akizungumziwa sana huku akitukanwa, akipondwa sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kitendo chake cha kupost picha ambazo zilikuwa zikimuonyesha sehemu kubwa ya mwili wake, licha ya yeye kukiri kuwa ametumia sanaa yake kubuni kitu ambacho kimebeba ujumbe wa kazi yake hiyo mpya ameamua kutoa shule kwa baadhi ya watu katika utumiaji wa mitandao ya kijamii.

"Hakuna tuzo inayotolewa kwa wanaotumia vibaya mitandao (kama vile kuchochea ma ugomvi, kutukana watu) Unawabeza na kuwaponda watu ambao wameshatimiza ndoto zao na wanaziishi, unasahau kwamba uko kwenye Account yake, kitendo cha kuwa kwenye Account yake ndio Ushindi wake, mbona yeye haingii kwenye 'Account' yako? It means you are No body. Work, please please Let's Work tufikie malengo tuliyojiwekea" alisema Ben Po

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com