Mama mjengo, Zari amevunja ukimya na kuamua kuweka wazi hisia zake kwa kuguswa na maradhi yanayomsumbua Mzazi mwenzake ‘Ivan Ssemwanga’ kwa kumuombea apate afya njema kama alivyokuwa zamani.

Zari kupitia ukurasa wake wa SnapChat ameandika “Siku mbili kwangu zimekuwa ngumu, nawaomba tumuombee Ivan”.

“Last 2 days have been hard. Let’s pray for IVAN please!“ameandika Mrembo Zari kwenye ukurasa wake wa Snapchat.

Taarifa kutoka mtandao wa Watch Dog wa Uganda umeripoti kuwa Ivan anasumbuliwa na maradhi ya Shambulio la Moyo (Coronary Artery Disease) .

Zari ambaye kwa sasa yupo kwenye mahusiano na Diamond Platnumz, amezaa na Tajiri Ivan Ssemwanga watoto watatu wote wa kiume.

Ungana nasi Facebook Like page yetu hapa chini

Weka Maoni Hapo Chini Kuhusu Habari Hii

Facebook Blogger Plugin by Celebrity Swaggz

Post a Comment

 
Top