Meneja Maneno ambaye ameanza kufanya muziki huku akiendelea kuwasaidia wasanii kusimamia kazi zao akiwepo Nay wa Mitego, amefunguka na kusema rapa huyo si mkorofi kama ambavyo watu wanamchukulia huku akidai Nay havuti bangi wala kunywa pombe.
                                                                    
                                                                                                              Meneja Maneno alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha eNewz ya EATV na kusema toka ameanza kusaidiana na Nay wa Mitego katika kazi hajaona ukorofi wowote ule kwake bali watu wamekuwa na dhana kuwa mkorofi kutokana na tungo zake katika muziki wake. Ambazo zimekuwa na utata na kuleta shinda kila anapokuwa akiachia ngoma.

"Nay si mkorofi kabisa sababu kwanza yeye havuti bangi, hanywi pombe hivyo ni mtu mmoja poa sana, sema tungo zake katika muziki ndiyo zinafanya watu kuhisi ni mkorofi lakini ni mtu poa sana" alisema Nay wa Mitego.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com