Msanii wa bongo fleva Belle 9 mwenye 'hit song' ya 'Ma Ole' alioshirikiana na G Nako amefunguka kwa kusema hawezi kufanya 'promo' ya kutangaza muziki wake kwa kupiga picha zitakazo kuwa zinamuonesha mwili wake kama alivyofanya Ben Pol hivi karibun
Belle 9 upande wa (kushoto), Ben Pol (kulia)

Belle amebainisha hayo kupitia kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV kila siku ya Ijumaa kuanzia saa tatu kamili usiku mpaka saa tano za usiku.

"Kwa maadili ya kiafrika na kwa jinsi ambavyo tumezoea sio kitu cha kawaida ninaweza sema lakini sijui labda anaweza akaja kutengeneza sababu ambazo zitaendana na zile picha...Kiukweli mimi siwezi, Siamini katika hilo kuwa muziki wa Ben Pol umeshindwa na upepo ila naona kama ameenda 'speed' kidogo...Ben Pol ana ujasiri mkubwa " alisema Belle 9.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com