AMA kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni! Wakazi na watumiaji wa barabara ya Pasiansi Jijini Mwanza, jana jioni walipigwa butwaa baada ya kushuhudia kimbwanga ajabu cha mti kutoa sauti kama binadamu ukipinga using’olewe.

Tukio hilo limetafsiriwa kuwa la kishirikina ama mazingaombwe ikizingatiwa kwamba si jambo lenye uhalisia mti kuongea kama binadamu.

Katika eneo la Pasiansi Jijini Mwanza mradi wa upanuzi wa barabara inayoelekea katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza unaendelea.

Shughuli ya kuung’oa mti huo aina ya mwembe bado inaendelea leo ambapo mamia ya wananchi wamejitokeza kushuhudia tukio hilo.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com