Baada ya minong'ono kuongezeka kwamba Muigizaji Shamsa Ford atamsindikiza aliyekuwa mpenzi wake Nay wa mitego kwenye tamasha la 'Wapo Tour' ya jijini Dar, Shamsa amekanusha kuhusu kushiriki katika show hiyo huku akidai hajui chochote

Shamsa amekanusha kuwepo katika show ya ‘Wapo Tour’ ya rapa Nay wa Mitego itayofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala, May 20, ikiwa ni siku chache kufikia kufanyika kwa tamasha hilo kwa madai kuwa hana tarifa rasmi ya kuhusishwa bali anaona kwenye mitandao tu akitajwa kuwepo.

Aidha amedai kuwa hajui chochote kuhusiana na show hiyo “Kusema kweli sina show yoyote na mtu na wala sijazungumza na Nay wa Mitego kuhusu show ya Dar Live".

Aliongeza,”Hajaniambia chochote siwezi kudanganya, ndio kwanza hizo taarifa naziona katika mitandao ya kijamii. Kama kweli na mimi nitakuwepo ungeona hata nikipost. Kwahiyo sitakuwepo kwenye hiyo show kwa sababu sina taarifa yoyote"- alisema Shamsa Ford

Wiki iliyopita rapa Nay wa Mitego alidai licha ya kuachana na muigizaji huyo na kuolewa na mtu mwingine lakini wanashirikiana katika mambo mbalimbali huku akimtaja Shamsa atakuwa MC siku ya show yake Dar live.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com