Aliyekuwa muimbaji wa muziki wa taarab nchini na mmiliki wa bendi ya Jahazi Modern Taarab, Mzee Yussuf ambaye aliamua kuachana na masuala ya muziki na kumrudia Mungu ameibuka sasa kwa kuanza kufanya biashara ya tofali.

Mzee Yussuf anasema ameamua kufanya biashara hiyo ya tofali za kujengea nyumba kwa kuwa Mungu ndiye amemtaka afanye biashara hiyo na si kitu kingine chochote

"Kwa hakika hii ndio biashara 'Allah' ametaka niifanye na mimi nimeanza kuizowea 'Alhamdulilaah' ukimtegemea 'Allah' hujutii licha ya majaribu na mirihani. Tupo chanika Taliani weka oda yako popote nakuletea"- alisema Mzee Yussuf.
Mradi wa Mzee Yusuph baada ya kuachana na uimbaji

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com