WAREMBO wawili ambao ni Video Queen, Gift Stanford ‘Gigy Money’ na Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ wameingia kwenye bifu zito baada ya Gigy kumtolea maneno machafu mwenzake na kusema kuwa anatakiwa kurudia kazi yake ya zamani ya u-baamedi.

Gigy alifikia hatua ya kumtolea maneno hayo Lulu kutokana na kauli yake aliyowahi kusema kwamba hataki kufananishwa naye kwa kuwa siyo levo yake kwa sababu hivi sasa ni mwanamuziki siyo video queen tena. Maneono ya Lulu yalimkera Gigy ambaye ameamua kumjibu kwa kumwambia kuwa anamtambua kama baamedi kwani hiyo ndiyo ilikuwa kazi yake hivyo anajiona yupo juu kwa kuwa alizoea kufunua visoda.

Baada ya Gigy kutoa maneno hayo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Lulu ambaye baada ya kuelezwa alijibu kwa ufupi; “Acha aongee maana huwezi kumkataza binadamu kuongea kwa sasa siwezi kujibizana na mtu wa aina hiyo anayetafuta kiki.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com