Kikosi cha Simba kimetua mjini Dodoma tayari kwa ajili ya mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho linalodhaminiwa na Azam Sports HD.

Mechi hiyo ya fainali dhidi ya Mbao FC inatarajiwa kuchezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini humo.

Simba ilikuwa kambini mjini Morogoro, lakini leo wamewasili tayari kwa kazi hiyo ya fainali.

Bingwa wa Kombe la Shirikisho anapata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com