Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kwamba kumetokea mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Shirika la habari la AFP limesema WHO imechukua hatua hiyo baada ya virusi vya ugonjwa huo kusababisha vifo vya watu watatu eneo hilo tangu Aprili 22.

WHO imesema mlipuko huo unaathiri maeneo ya msituni katika mkoa wa Bas-Uele karibu na mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Shirika la habari la Reuters, likimnukuu mmoja wa wasemaji wa WHO Eric Kabambi, akisema mtu mmoja amethibitishwa kufariki kutokana na Ebola.

"Ni kisa kilichotokea eneo lililo mbali sana, lenye msitu mkubwa, kwa hivyo tulikuwa na bahati kiasi. Huwa twachukulia kwa uzito sana visa kama hivi," alisema Kabambi.

Wizara ya afya nchini Demokrasia ya Congo imesema kisa hicho cha Ebola kilithibitishwa baada ya watu tisa waliokuwa na homa kali kutoka mkoa wa Bas-Uele kuipimwa.

Mwaka 2014, mkurupuko wa ugonjwa huo Congo ulidhibitiwa kwa haraka ingawa watu 49 walifariki.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com