Siku kadhaa zilizopita tuliangalia kwa uchache kuhusu faida za kula chungwa hivyo, pia siku ya leo naomba tuendelee kwa kuangalia faida nyingine za kula chungwa.

1. Ulaji wa machungwa husaidia kutibu mapafu.
Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.

2. Husaidia kuimarisha mifupa ya meno.
Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno.

3. Husaidia kupunguza kiwango cha mafuta mwilini.
Virutubisho vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake.

4. Hupunguza kupatwa magonjwa wa figo.
Ulaji wa machungwa mara kwa mara, ukusaidia kujiepusha na ugonjwa wa figo kwa kiasi kikubwa.

5. Chungwa husaidia kutibu vidonda vya tumbo.
Unapokuwa na kiwango cha kutosha cha Vitamin C mwilini, una uhakika na kinga dhidi ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo, na kama tayari unavyo, ulaji wa machungwa utakupa ahueni.

Hivyo ni heri ungazingatia ulaji wa kachungwa mara kwa mara, kwani yana faida lukuki katika mwili wako!

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com