Dogo Janja 'Janjaro ameibuka na kujigamba hakuna msanii yoyote hapa nchini Tanzania na ukanda wa Afrika ya Mashariki anayevaa na kupendeza kama yeye kwani wengi wamekuwa wakivaa na kufanana na Wakongo.

Msanii huyo amejigamba mbele ya kamera ya eNewz ya EATV na kusema kuwa yeye peke yake ndiye msanii anayevaa kinyamwezi, wengine wanavaa rangi nyingi kiasi cha kuweza kumzimisha hata kinyonga hivyo hapaswi kulinganishwa na wasanii wengine.

'"Mimi msinilinganishe na hao wasanii wengine wanaovaa nguo ambazo kinyonga akikutana nao wanaweza kukimbia. Hebu niangalie mimi sivai kama Mkongo navaa Kinyamwezi na katika wasanii peke yangu ndiyo ninavaa nikapendeza hata nikitokea mbele za watu sina haja ya kujitambulisha kuwa mimi ni msanii, muonekano wangu tu unatosha kukuelezea mimi ni mtu wa aina gani"- Dogo Janja.

Hata hivyo watu katika mitandao ya kijamii wameanza kuponda maneno hayo ambaye hata yeye ameyaandika katika mtandao wake kwa kuhisi anatafuta kiki ya kuachia wimbo mpya.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com