Meneja wa Yamoto Band, Chambuso amesema msanii Aslay hapendelewi kwenye kundi hilo kama wengi wanavyodhani kwa sababu linapokuja suala la solo project kwenye kunid hilo, kila mmoja anakuwa na management yake.

Chambuso amesema jinsi Aslay anavyoonekana akifanya vizuri na kazi zake yeye pekee yake, watu waelewe kuwa amefanya na management yake na Mkubwa na Wanawe haihusiki.

“Hapana, Aslay anafanya kazi pekee yake na management yake, pia Maromboso atakuwa anafanya na management yake na watakuwa na vikao vyao na kushauriana jinsi ya kutoa nyimbo na hao wengine,” Chambuso amekiambia kipindi cha Daladala Beat na kuongeza.

“Unaona kama wimbo wa Beka, Mkubwa na Wanawe hatujahusika. Ni yeye na management yake ndio wametoa, kwa hiyo sidhani kama Aslay anapendelewa kwa sababu kila mmoja ana management.

“Hakuna mtu anayependelewa, sisi kama uongozi wa Yamoto tunafanya vitu kwa usahihi, kama Aslay anastahili kulipwa laki atalipwa, na kila mtu alikuwa anaandika verse mwenywe hakuna mtu aliyekuwa anaandikiwa verse, kwa hiyo kila mtu alikuwa anapewa nafasi kufanya kile alichokuwa anafikiria,” ameeleza Chambuso.


0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com