Msanii  wa muziki wa bongo fleva mwenye makazi yake Zanzibar, Baby J ameweka wazi kwamba amekuwa kimya kuachia kazi mpya hivi karibuni baada ya kuharibiwa video yake na 'director' Hanscana hivyo kwa sasa yupo jikoni kuandaa kazi nyingine nzuri.

Baby J amefunguka hayo kwenye Planet Bongo ya EATV na kusema kwamba alishindwa kuachia video aliyofanya na muongozaji huyo kwa sababu hakupenda jinsi ambavyo video ilivyokuwa imehaririwa kana kwamba ilifanywa kwa haraka haraka huku akiongeza kwamba haikuwa kama jinsi alivyotaka ndiyo sababu akaamua kuipiga chini.

"Ni kweli najua mashabiki zangu wamenimiss na wanataka kunisikia lakini siwezi kuwapa kitu ambacho siyo bora, hata wakiwa mbele za watu washindwe kusema kama wao ni mashabiki zangu kwa nini? kwa sababu naachia kazi mbovu? ndio maana nikaamua kukaa kimya. Video niliyofanya na Hanscana sikuipenda, hai ku-editiwa kama nilivyotaka sijui alikuwa na haraka au vipi. haikuwa mbaya lakini kwangu sikuipeda hivyo mashabiki zangu niwaombe wanisubiri siku siyo nyingi Mungu akijaalia nitaachia tuu kazi nzuri"- Baby J

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com