HATIMAYE Pacha walioungana wilayani Kilolo Mkoani Iringa wamehitimu elimu yao ya sekondari ya Kidato cha sita huku wakiiomba serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kuwasaidia mitaji ya biashara ambao itawasaidia kujiendeleza na kujikwamua kimaisha.

Pacha hao Maria na Consolata waliwasilisha ombi hilo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asiah Abdalah alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga.

“Tumehitimu elimu yetu ya sekondari ya kidato cha sita, lakini tunaomba wasamaria wema watusaidie mtaji wa biashara wakati tukisubiri matokeo ya kuendelea na elimu ya chuo kikuu, sisi wenyewe tunavipaji tunaweza kufuma,kuchora na kudarizi na tukipata mitaji hiyo itatusaidia hata kujiendeleza kwa mambo mengine,’walisema.

Naye Mkuu wa Wilaya Asiah aliwaasa wanafunzi waliohitimu elimu yao kupiga vita rushwa inaangamiza taifa, inadhulumu haki hivyo watu wote wanatakiwa kupinga rushwa, na dawa za kulevya.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com