MWIGIZAJI wa filamu za Bongo, Jackline Wolper, ameweka wazi kwamba pombe ndiyo inayomsababishia unene anaopigania sasa kuupunguza.
Wolper alisema watu wengi wanadhani ulaji wa chakula zaidi ndiyo unaosababisha mwili wake kuwa mnene kiasi cha kutowavutia baadhi ya mashabiki wake lakini ukweli ni kwamba unene huo unasababishwa na unywaji zaidi wa pombe.
“Unajua sikuwa mnywaji na nilikuwa nikiichukia pombe sababu nikinywa ndio napata hamu zaidi ya kula chakula kingi, hivyo kwa sasa nimeanza harakati za kurudisha mwili wangu wa mwanzo uliokuwa ukinionyesha vizuri kwa mashabiki wangu na pia nipo kwenye harakati za kuachana na unywaji wa pombe,” alieleza.
Mtanzania

Ungana nasi Facebook Like page yetu hapa chini

Weka Maoni Hapo Chini Kuhusu Habari Hii

Facebook Blogger Plugin by Celebrity Swaggz

Post a Comment

 
Top