Rapa Harmorapa jana aliwaacha mdomo wazi baadhi ya mashabiki wake baada ya kutoa jibu tofauti kuhusu jinsia yake.

Akichat na mashabiki katika mtandao wa facebook wa EATV ndani ya kipindi cha  Kikaangoni, rapa huyo aliulizwa swali kuhusu jinsi yake "Wewe ni mwanaume wa aina gani?' na rapa huyo kujibu "Mimi ni strong woman".
Jibu hilo limewashangaza mashabiki wengi wa rapa huyo kwa kuwa wanajua yeye ni mwanaume huku wengine wakidhani huenda hakuelewa swali kutokana na lugha ya kingereza iliyotumiwa.

Akiongea kuhusu uwezo wake wa kuongea na kuandika lugha ya kingereza alisema: “Lugha ya Kiingereza naifahamu vizuri lakini ile kuongea ongea ndiyo siwezi”

Rapa huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Kiboko ya Mabishoo’.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com