Harmorapa amefunguka kwa kuwataja mastaa waliosababisha kutumia jina analotumia sasa kwenye muziki.
Akingea kwenye kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM, rapper huyo amemtaja Roma na Mr T-Touch kuwa ni watu ambao walimshauri kutumia jina la Harmorapa.
“Baadhi ya mastaa wakubwa katika muziki wa hapa Bongo nao walinishauri nijiite hivi, akiwemo brother Roma Mkatoliki na Mt T-Touch,” amesema rapper huyo.
Harmo ameongeza kuwa kabla ya kutumia jina hilo alikuwa akifahamika kwa jina la Jembe la Kusini.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com