Msanii kutoka TMK Wanaume Family, Chege Chigunda amesema yuko mbioni kukata kiu ya mashabiki wa 'Chege na Temba' kwani bada ya kutoa ngoma yake ya Kelele za Chura, ngoma inayofuata ni yake na swahiba wake Mh. Temba kutoka familia hiyohiyo ya Wanaume.

Chege amelazimika kuweka wazi hatma ya Chge na Temba kutokana na kukumbana na maswali mengi ya watu mbalimbali wakitaka kujua ni lini wasanii hao watafanya tena kazi ya pamoja kutokana na temba kuwa kimya kwa muda mrefu.

Chege aliyekuwa akiitambulisha rasmi 'EXCLUSIVE' video yake ya 'Kelele za Chura' kwenye kipindi cha Friday Night LIVE cha EATV, alisema kwa sasa na yeye ameamua kutoa albam kwa kuwa anaamini albam zina soko, na kwa kutambua wabongo wame-miss albam kwa muda mrefu, sasa ameamua kukata kiu ya mashabiki.

Ameitaja albam yake kuwa itakwenda kwa jina la 'Sweet Sweet' na itakuwa na nyimbo 15, na kwamba kila kitu kimekamilika, na katikati ya mwezi huu itakua madukani

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com