POLISI mkoani Simiyu, Oliver Paschal (39), mkazi wa Kijiji cha Ipililo katika Kata ya Mwagala wilayani Maswa, kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo yenye uzito wa kilo 32 akiwa ameyaficha uvunguni mwa kitanda chake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Onesmo Lyanga alisema Polisi baada ya kupata taarifa za kiintelenjinsia, walimkamata mwanamke huyo akiwa na pembe mbili za ndovu alizokuwa amezificha chini ya uvungu katika chumba alichokuwa akiishi.

Kamanda Lyanga alisema mwanamke huyo alikamatwa Novemba 11, mwaka huu saa tisa alasiri na kueleza kuwa alikamatwa na meno hayo yenye uzito wa kilo 32 katika chumba alichokuwa amepanga kwenye nyumba ya Edward Malanda.

Aidha, kamanda huyo amesema kesi zaidi ya 86 zinazohusu ujangili zimesharipotiwa kuanzia Januari hadi Septemba 2015, wakati kesi 69 zimesharipotiwa Polisi kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo linawashikilia watu wanane kwa kosa la kujichukulia sheria mkononi kwa kumpiga na kumuua kwa mawe na marungu, Manoni Elisha (38), mkazi wa Kijiji cha Ngasamo wakimtuhumu kuwa ni mwizi.

Lyanga alisema saa 3 usiku katika baa ya Manchester iliyopo Ngasamo wilayani Busega, watuhumiwa hao walimuua mtu huyo kwa tuhuma za makosa mbalimbali, ikiwemo wizi wa kondoo kwa kesi namba NGAS/IR/49/2016 ambayo alikuwa akitafutwa na Jeshi la Polisi.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com