Msanii wa muziki ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo ‘Binti kiziwi’, Z Anto amefunguka na kusema kuwa mpaka sasa kuna label zaidi ya nne ambazo zinamuhitaji kufanya naye kazi lakini amekataa kufanya nao kazi.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo kimya, amesema alipata ofa ya kujiunga na WCB lakini alikataa kwa kuwa yeye mwenyewe anadai anatamani kufanya kazi nje ya WCB.

“Unajua mimi tatizo langu huwezi kufanya kazi kwa kubahatisha, mpaka saizi kuna ‘label’ nyingi zaidi ya tano zinanihitaji kufanya kazi, hivyo sipendi kukurupuka lazima nitulie nione nawezaje kujiunga na moja kati ya hizo. Maana nikibugi kuchagua ‘label’ ambayo inaweza kunisimamisha kufikia pale napotaka mimi nitakuwa nimejimaliza mwenyewe. Nilikuwa na maongezi na Babu Tale, nikapewa ofa kurekodi na kujinga WCB, lakini mimi natamani kufanya kazi nje ya Wasafi, nipo tayari kufanya kazi na Tip Top Connection” Z Anto alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV.

Akieleza sababu ya kukataa ofa ya kujiunga WCB, Z Anto alisema “Sisi ni washairi ujue na siku zote mafahari wawili hatuwezi kufanya kazi sehemu moja, nachoweza kuwaambia ni kwamba ukimya wangu una mambo mengi mazuri na saizi kuna label moja kubwa ambayo mimi natamani kwenda kufanya nao kazi na mambo yanakwenda sawa nitakaribia kuanza nao kazi muda si mrefu,’ alisema Z Anto

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com