Dodoma. Serikali imeunda timu ya watu 10 ambayo itashirikiana na wataalamu kutoka China na Malaysia, kupitia upya mpango kabambe (master plan) wa mji wa  Dodoma ili kuepusha makosa kama yaliyojitokeza Dar es Salaam.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa umma  mjini hapa, baada ya ziara yake ya kutembelea maeneo ya kutolea huduma ikiwamo zahanati, hospitali na shule.

Ziara hiyo ya siku mbili aliyoanza jana, inalenga kukagua hatua mbalimbali za maandalizi ya ujio wa Serikali mjini hapa.

“Tumeunda timu ya watu 10 ambao ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa miji mikuu, hawa wana uzoefu wa kuangalia makao makuu ya nchi yanafananaje. Watakuja Dodoma wapitie master plan  kisha watapita maeneo kadhaa ya mji ili waone hali halisi watupe maoni yao,” alisema.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com