Serikali ya Tanzania na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), wametiliana saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wao katika nyanja mbalimbali ikiwemo suala la ulinzi na usalama pamoja uchimbaji wa mafuta katika ziwa Tanganyika.

Akiongea leo Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais Joseph Kabila, Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa pamoja na mambo mengine wamekubaliana ushirikiano wa kimaendeleo katika uwekezaji pamoja na jinsi ya kusimamia uchaguzi ujao wa nchi hiyo kupitia uongozi wake katika nchi za Jumuiya ya nchi za SADC.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa mbali ya kuangalia masuala ya kiusalama nchini humo pia amemuomba wafanyabiashara kutoka nchini Congo kuja kuwekeza nchini pamoja kutumia bandari ya Dar es Salaam kwa katika usafirishaji wa bidhaa.

Rais Magufuli amesema kuwa wamekubaliana na mamlaka ya bandari kuongeza muda wa mizigo inayokaa bandarini mpaka muda wa siku 30 badala ya siku 14 kama ilivyo awali huku akiongeza kwa kusema kuwa hata ujenzi wa reli ya Standard Geuge utaifaidisha Congo katika usafirishaji wa mizigo.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Joseph Laurent Kabila amesema kuwa anaamini ushirikiano huo utakuza maendeleo ya pande zote mbili pamoja na nchi za jumuiya ya SADC ikiwa ni pamoja na kufanya uchaguzi utakaozingatia demokrasia nchini humo.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com