Tuzo za AFRIMMA ambazo hutolewa kila mwaka kwa Waafrika mbalimbali waliofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali hasa za burudani, zimetolewa Dallas Texas Marekani leo ambapo kwenye list yote Watanzania walioshinda ni watatu.

Watanzania walioshinda ni Dj D Ommy wa CloudsFM kupitia show mbalimbali ikiwemoXXL na AMPLIFAYA ambapo ameshinda tuzo ya Dj bora Afrika, mwimbaji Harmonize akishinda tuzo ya msanii bora chipukizi Afrika 2016 huku Diamond Platnumzakishinda ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki.

Sasa miongoni waliotoa pongezi kwa Harmonize ni Diamond Platnumza ambae kupitia instagram alipost picha na kuyaandika haya>>>>hii picha inanikumbusha mwaka jana ulipokuja nipokea airport kutokea@afrimma …ukaniuliza “hivi ipo siku nami nitachaguliwa tunzo yoyote ya kimataifa”….nikakwambia “Ukifanya kazi kwa bidii’

‘Ukimuheshimu kila mtu, ukamuamini na kumuomba Mwenyez Mungu basi Mollah atakufungulia ndoto zako….na leo hii kweli Tunafurahia Ushaindi wako wa Msanii Bora Chipkizi Africa….. Hongera sana @harmonize_tzna shukran sana sana kwa Mashabiki zetu pendwa kwa kura na @Afrimmakwa kuendelea kuvinyanyua vipajia vya Africa🙏’-Diamond Platnumz

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com