Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Tunda Man pamoja na mpenzi wake wa muda mrefu wamefanya ‘send-off’ wakijiandaa kuingia katika maisha ya ndoa.

Alhamisi hii usiku zilisambaa picha katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha Tunda Man pamoja na mpenzi wake wakiwa kwenye ‘send-off’.

Mmoja kati ya wasanii ambao walihudhuria shughuli hiyo ni Dojo Janja ambapo alimpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo.

“From❤️ congrats my big brother captain @tundamantz. Kesho tunabeba jiko letu mapema mapema tu, hatucheleweshi mambo. Mimi ninao wengi sijui nioe yupi,” aliandika Dogo Janja Instagram.

Wiki chache zilizopita, muimbaji huyo wa wimbo ‘Mama Kijacho’, aliiambia Bongo5 kuwa atafunga ndoa hivi karibuni.

“Kusema kweli suala la kuoa naoa hivi karibuni. Kwa hiyo mtu yeyote anakaribishwa na nipo tayari kuingia kwenye maisha ya ndoa,” alisema Tunda Man.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com