Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda amesema kuna watu wanaohoji wakiwemo mawaziri kuwa anatafuta nini?

Yeye amesema hawezi kujizuia na anawajibu kuwa anatafuta kutimiza kusudi la Mungu kwenye nafasi aliyopewa, na kingine ni kuwapa heshima waliompa nafasi aliyonayo

Amesema kuna watu wengi walikuwa wanaongea kuhusu yeye kupewa nafasi ya ukuu wa mkoa wakati yeye ni mdogo na hataweza lakini licha ya hayo rais akamuamini na kumteua

Lingine amesema anataka aache alama kuwa kuna mtu alikuwa mkuu wa mkoa wa Dar na akafanya mambo kadhaa

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com