Nay wa Mitego amedai kuwa kinachoendelea kati ya Barakah The Prince na Stan Bakora, kinaweza kuwa kitu cha kutengeneza.

Akiongea na mtangazaji wa Kings FM, Prince Ramalove, rapper huyo amewaita wawili hao wote watoto na kwamba umri wao unawaruhusu kufanya wwanachokifanya.

“Siwezi kusimama upande wowote, hao ni watoto, wote ni wadogo mimi ni wadogo zangu,” alisema.

“So inapofika time wanagombana wataelewana tu. Hatuwezi kujua labda ni kiki, haiwezi kuwa beef kiasi hicho, inawezekana labda kiki, watu mkachukulia serious kumbe wamekaa wametengeneza,” ameongeza Nay.

Barakah ameonekana kuchukizwa na parody aliyofanya Stan ya wimbo wake Nisamehe ambapo amejipaka masizi usoni kuwa mweusi kama muimbaji huyo.

Stan amejipatia umaarufu kwa kuigiza sauti ya Nay wa Mitego

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com