Muimbaji nguli wa Tanzania aliyetamba na vibao kama Mapenzi Kizunguzungu, Kitobero na nyingine nyingi amesema kuwa ana hofu ya kuwa na meneja kwa sasa kutokana na yaliyomsibu miaka kadhaa nyuma.

Najua, kuna mameneja wazuri katika muziki wa bongo kama meneja wa Diamond Platnumz hata wa Ali kiba. Lakini kuna baadhi ya mapromota na mameneja kwa kweli nina wahofia sana. Alisema Saida Karoli.

Saida Karoli ameeeleza kuwa wakati wake alifanya vizuri sana kimuziki lakini hakuona mafanikio hayo kifedha. Hayo yote ni kutokana na uongozi wake.

Amesema kuwa hata sasa akipata meneja mwingine atahakikisha anajiridhisha kwanza kama anaweza kazi ndio aingie nae mkataba. Saida Karoli amesema jina lake kwenye jukwaa ni kubwa sana kuliko mafanikio aliyonayo, na hii humfanya aamini kuwa alitumika kuwanufaisha watu wengine.

Nilikuwa nikilipwa fedha kidogo sana kutokana na kazi zangu za muziki. Kama mwandishi akitembelea ninapoishi Watanzania wataweza kuelewa ni nini ninazungumzia.

Muziki wa Saida Karoli bado unaendelea kuishi na kuvutia watu mbalimbali licha ya kuwa uliiimbwa miaka mingi nyuma. Diamond Platnumz aliurudia wimbo wake wa Salome na kuongeza vionjo ili kuuboresha na Saida Karoli atapata asilimia 25 ya mauzo yote ya wimbo huo.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com