Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama Cha wananchi CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba ametengua uteuzi wa wakurugenzi na manaibu wao sita kwa kile alichokiita ni kutokana na changamoto zinazokikabili chama hicho.

Wakurugenzi waliotenguliwa uteuzi wao ni pamoja na Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha, Joran  Bashange, wa Mambo ya Nje Ismail Jussa Ladhu, Ulinzi na Usalama Mustafa Wandwi, na Haki za Binadamu na Sheria Kulthum Mchuchuli.

Amewataja manaibu aliotengua uteuzi wao kuwa Shaweji Mketo, Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi na Abdalla Mtolea, Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje

“Niliteua Wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa tarehe 28 Juni 2014 kunichagua kuwa Mwenyekiti wa Taifa....na kwa kuzingatia changamoto zinazokikabili Chama chetu hivi sasa, nimeamua kutengua uteuzi wao” amesema Profesa Lipumba.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com