Saa chache baada ya kusambaa taarifa zilizokanushwa na Ikulu zilizodai kuwa uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo umetenguliwa, Mkuu huyo wa Mkoa ameandika ujumbe mzito unaoonekana kuwalenga mahasimu wake.

Taarifa hizo zilizothibitishwa kuwa za uongo ziliibuka siku moja baada ya tukio la kusikitisha la kuzuka ugomvi wa maneno kati ya Mkuu huyo wa Mkoa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwenye hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya Burka nje kidogo ya jiji la Arusha, mbele ya wafadhali wa mradi huo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Gambo ameandika, “Mara nyingi ukisikia huyu ana kufa leo au kesho, huwa anaishi miaka mingi zaidi! Nazungumzia utamaduni wetu sisi Watanzania!”

Mvutano kati ya Gambo na Lema ulianza tangu Gambo alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha huku kila mmoja akimtupia lawama mwenzake kwa kutofuata taratibu na protokali.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com