Tokeo la picha la jerry muroMTAZAMO WANGU

Nimesoma hoja za wadau tangu juzi na jana, nimeona na kujifunza mengi sana kutoka kwa waliokuwa viongozi wa yanga na wadau wa yanga kuwepo kwa tofauti ya mitazamo ni jambo la afya katika uhai na maendeleo ya Yanga hilo kwanza lazima tukubaliane.

Nichangie kidogo hapa mimi kama Jerry muro nachangia kama mdau wa kawaida tu kwa tulipofika sasa lazima tukiri kuwa tunaitaji club iongozwe na watu wenye mitaji mikubwa ya fedha iwe kwa kukodishwa au kuwekeza mana mfumo wa uendeshaji wa mpira duniani kote umebadilika kasoro Tanzania ambapo bado tuko kama vile kwenye soka la ridhaa wakati mfumo unaotawala ni soka la kimataifa na la kisasa.

Vilabu vya Tanzania vimekuwa kama vile ni vijiwe vya kufurahishana tu baada ya kazi na haswa kwa simba na y
Yanga vikishafungana vyenyewe kwa vyenyewe biashara imekwisha hakuna kifuatacho, na ndio mana tunapokwenda kwenye michuano ya kimataifa tunapata shida mana sisi mtazamo wetu ni yanga amfunge simba basi mtaani tushikishane adabu kwisha kazi.

Sasa tunachotakiwa ni kutoka hapa tulipo na kwenda mbele zaidi kwa kuwa na mfumo na muundo thabiti wa kimataifa.
Kwa Yanga tumeanza na tunashukuru Mungu tumeanzia pazuri kwa kuwa sasa muamko umekuwa mkubwa na umejenga mijada mingi sana ya kuonyesha dira ya tuendako, hilo kwangu mimi ni afya kubwa sana kwa maendeleo ya Klabu.

Tusiwabeze waliothubutu tuwasaidie kwa kuwaonyesha njia na kuwatia moyo mana tukumbuke kila jambo Kiowa linaloanza kwa mara ya kwanza lina changamoto kubwa zipo nyingine zinaweza kutatulika kwa sasa na haswa kwenye mikataba na yako mengine yatakuwa yanajitatua taratibu yenyewe wakati mfumo na muundo unaendelea cha msingi ni kuwa na SUBIRA.

Mwisho nimalize kwa kusema kuwa hizi ni zama mpya zenye maono mapya na mwamko mpya lazima tukubali kubadilika la sivyo tutabadilishwa kwa lazima(nature will change us)
Kwa wale wenye nia pia ya kusaidia yanga bado fursa zipo nyingi sana katika maeneo mengine makubwa mfano mali za yanga majengo, kuwekeza kwenye rasilimali watu ambao ni wanachama na mambo mengine, na tukiona hatuwezi uko basi tuvute subira tusubiri baada ya miaka 10 tujitokeze kuchangamkia fursa kutoka Yanga.

Niseme kutoka moyoni kabisa Yanga ni yetu sote tusaidiane kuijenga yanga na sio kuibomoa na katika yote lazima tukubali kuvumiliana katika madhaifu yetu hakuna mkamilifu chini ya mbingu na jua hivyo KUVUMILIANA NI JAMBO LA BUSARA SANA.

Jerry Cornel Muro
Mdau wa soka Yanga

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com