Rapper Mwana FA aka Binamu amezitaja nyimbo zake tatu ambazo anazikubali kwa mwaka huu kutoka Bongo

Hitmaker huyo wa Asanteni alikuwa akijibu swali la mmoja wa mashabiki wake kwenye mtandao wa Twitter, lililokuwa linauliza “Nitajie ngoma tatu za kibongo ambazo ni bora kwako kwa mwaka huu toka uanze?”

FA alijibu swali hilo kwa kuandika, “Aje, Chafu Pozi na Too Much.”

Wiki iliyopita wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Campus Vibes cha Times FM, Binamu aliwataja Bill Nas na Darassa ndio rapper anaowakubali zaidi kwenye kizazi cha sasa.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com