Msanii wa Hip Hop Bongo, Bill Nas amefunguka juu ya tetesi za kuhusishwa kujiunga na lebo ya WCB.
Tokeo la picha la bill nass
13258841_1713378792244504_924629682_n
Akiongea na kipindi cha Clouds E cha Clouds TV, rapper huyo amesema kuwa taarifa hizo si za kweli.
“WCB ni lebo kubwa kwasasa Afrika Mashariki nadhani hilo lipo wazi kabisa ila swala la mimi kwenda Wasafi aisee hata mwenyewe nimeshangaa, maana hata sijawahi kuongea na uongozi wa WCB wala sijawahi kwenda hata studio kwao, naona limekuwa kubwa hadi washikaji zangu wananipigia simu wakiniulizia lakini si kweli kabisa hilo swala,” alisema Bill Nas.
Kwasasa Bill Nass anafanya vizuri na ngoma yake Chafu Pozi.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com