Spidi ya Diamond kulitafuta tobo la Marekani inatisha. Akiwa na collabo kibindoni na French Montana, Yo Gotti na Ne-Yo ambaye watakuwa na ziara ya pamoja Uingereza Disemba mwaka huu, muimbaji huyo wa ‘Salome’ ametoa hint ya mradi mwingine ujao na role model wake mwingine – Usher.

Ametoa hint hiyo Ijumaa hii wakati akimpongeza muimbaji huyo wa ‘No Limit’ katika siku yake ya kuzaliwa.
“Happy Birthday Bro… Can’t wait for our Big day! @usher,” ameandika kwenye Instagram.
Kwa muda mrefu Diamond amekuwa akiwataja Ne-Yo na Usher kuwa ni watu anaowaangalia sana.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com