Mfanyabiashara kijana, Mohammed Dewji (MO) amefanikiwa kushinda tuzo kutoka Taasisi ya Choiseul ya nchini Ufaransa kama mfanya biashara kijana ambaye anasaidia kukuza uchumi wa bara la Afrika.
Tokeo la picha la moha,ed dewj
mohammed-dewji
Mo ameshinda tuzo hiyo ambayo aliwashinda wafanyabiashara wengine vijana 100 wenye asili ya Afrika ikiwa ni mara ya tatu kushinda tuzo hiyo tangu taasisi hiyo ianze kutoa tuzo hiyo.
Choiseul imesema kuwa Mohammdei Dewji amekuwa akijihusisha kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko na kutoa nafasi kwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi jambo ambalo limeleta matumaini mapya kwa Tanzania na Afrika kuweza kufika pale wanatamani wafike.
Kwa upande wake Mo amesema kuwa ataendelea na dhamira yake ya kuisaidia Afrika kupitia biashara anazozifana.
“Ninafuraha kupokea utambuzi huu kwa ajili ya kazi ambayo nimekuwa nikifanya katika bara la Afrika. Katika safari yangu ya ujasiriamali, nitaendelea kujikita kufanya biashara, kwa kupitia MeTL, nitaendelea na dhamira yangu ya kuendeleza Afrika kupitia sekta binafsi kwa kuleta maendeleo,” amesema Mo.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com