Ukimwaga mboga wenzio wanamwaga ugali.
Ukweli wafahamika baada ya mara kadhaa Rapper Young Dee
kukanusha kuwahi kuwa na mahusiano na video vixen
kutoka kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Amber Lulu.

Akiongea na U-Heard ya Clouds FM, Amber Lulu amefunguka
ukweli kwa kusema kuwa amekuwa na mahusiano na rapper
huyo kwa tangu miaka minne iliyopita wakati akiwa mkoani
Mbeya.

“Marafiki zangu wanajua ni jinsi gani nilivyokuwa naishi
naye, mara ya mwisho alikamatwa na polisi mimi ndio
nilienda kumtoa ndugu zake wote walikataa kwenda, Mimi
nimeenda. Matatizo yangu yeye anayafurahia ina maana.Sikuwa nimefanya vile kwa kuwa alikuwa ni mpenzi wangu ni
mtu ninayemfahamu siku nyingi na ambaye tupo wote,”

Amesema Amber.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com