ikiwa ni baada ya mwimbaji staa wa Marekani Chris Brown kufanya show weekend iliyopita Mombasa, mpya ya leo imetoka kwa Gavana wa Mombasa Hassan Joho ambaye inaelezwa ndiye alidhamini tamasha la Mombasa Rocks Music Festival.

 Story kutoka 254 Kenya zinasema Gavana huyu inayedaiwa ana pesa za kutosha, ametangaza kuwa timu yake imeanza mazungumzo na uongozi wa rapper Nicki Minaj ili aje Mombasa kutumbuiza hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Nairobi Wire, Jamal Gaddafi aliyekua MC kwenye tamasha la Mombasa Rocks  Music Festival amesema amepewa taarifa na Joho, awambie mashabiki wajiandae kwa show nyingine kubwa ya Nicki Minaj.

Ripoti kutoka Kenya zinasema sababu kubwa hasa ya Gavana huyo kuwaleta mastaa wakubwa kutoka Marekani ni kutaka kukuza jina lake na kuitangaza zaidi Mombasa kwenye suala la utalii.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com