Msanii wa muziki ambaye ni zao la Fiesta Super Diva 2014, Ruby, amesema wimbo ‘Wale Wale’ sio dongo kwa mtu yeyote bali amemwimba shetani.

“Mimi sijaimba huu nyimbo kwa ajili ya mtu yeyote kama ambavyo watu wanaweza kufikiria,” alisema Ruby. “Hii ni inspirational song, sijaimba mapenzi kabisa humo ndani kama ambavyo watu wanavyomuongelea Ruby anaimba mapenzi tu. Halafu sijamwongelea mtu nimemwongelea shetani, sifa za shetani,”

“Shetani siyo mtu wala hajafanana na mtu ila ni roho ambayo inaweza ikamwingia mtu yeyote. Hiyo roho inaweza ikaplay part mbili tofauti, hiyo roho inaweza ikakuletea kitu kizuri kumbe inataka ikitawale halafu ikuharibie, lakini kitu kizuri na chakudumu nichamungu.

Na hivyo hivyo hivi vitu vinatokeaga kwa mabosi wetu, pengine bosi akakutaka kimapenzi ili akupandishe cheo, lakini ile hali siyo hali nzuri, kwa hiyo mimi sijamwongelea mtu yeyote bali ni shetani ambaye mara nyingi anataka kutuaribia maisha yetu,” aliongeza.

Wimbo ‘Wale Wale’ ni wimbo wake wa kwanza kuuandika mwenyewe toka aanze kufanya muziki.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com