Baada ya kutotajwa jina lake kwenye tuzo za MTV MAMA 2016, Davido amejipa moyo kufanya vizuri mwakani kwenye tuzo hizo.

davido

Kupitia mtandao wake wa Twitter, muimbaji huyo ameandika, “I really shouldn’t be nominated this year For what?? I got three MAMAS in two years I’m good ! Still gonna be a great show! BUT NEXT YEAR 😈.”Davido amefanikiwa kushinda tuzo tatu za MTV MAMA ndani ya miaka miwili mfululizo huku tuzo mbili kati ya hizo zikiwa ni ‘Best Male’ alizoshinda mwaka jana na mwaka juzi.

Tangu staa huyo aliposaini mkataba na kampuni ya Sony Music mapema mwaka huu mambo yameonekana kumwendea kombo huku akiwa hajaachia wimbo hata mmoja na kuvunja mara kadhaa ahadi yake ya kuachia albamu yake iliyotakiwa kutoka tangu mwaka jana.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com