Kampuni ya Google imekuja kufanya mapinduzi kwa kuzindua App yake mpya “Google Allo”
Google Allo ni app ambayo imetengenezwa na kampuni ya google kwa ajili ya kuchati kama zilivyo app zingine kama Whatsapp, Hangout, Messenger, Imessage na zingine kibao, lakini App hii imekuja na uwezo maalumu ambao unakuwa unatambua tabia ya mtu anavyochati kila siku, kujibu meseji zako na mwisho inakuwa na uwezo wa kukusaidia kujibu jumbe zako kutokana na ujumbe ambao unakuwa umeupokea.Kitu kingine ambacho pia unapaswa kukifahamu kuhusu App hii ni kwamba, Allo inatumia namba kama ilivyo Whatsapp kwamba mtu hawezi kukuona mpaka awe na namba yako, kizuri zaidi ambacho mtumiaji wa App hii anaweza kufurahia ni kwamba Allo imeundwa na Google assistant ambaye anakuwa anakusaidia kila swali na kitu chochote ambacho unahitaji kukifahamu katika mtandao, yaani mtumiaji unakuwa hupati shida kuingia google na kutafuta vitu.

Allo inapatikana pia kwa watumiaji wa simu za Iphone na Android, App imekuja kufanya mapinduzi makubwa kwa Whatsapp, ni moja ya App ambayo haina mbwembwe nyingi katika kujiunga na ni nyepesi kushinda whatsapp hata ufanyaji kazi wake nao ni mwepesi.
Ipakue sasa ili na wewe uwe wa tofauti katika maswala ya teknolojia

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com