Dada yake Diamond, Esma Platnumz ameungana na mama yake, Bi Sandra kukitia chumvi kidonda cha Zari The Boss lady.
Amempongeza wifi yake wa zamani, Wema Sepetu katika birthday yake Jumatano hii ikiwa ni siku chache tu baada ya kumlia buyu wifi yake wa sasa Zari ambaye naye alisherehekea siku yake ya kuzaliwa siku chache zilizopita.
“Naona watu wengi hii pic wanaipenda anyways yaliyopita si ndwele wenyewe wa nakwambia kuwa mzalendo happy birthday to you love tulikupenda tunakupenda na tutazidi kukukumbuka wallah unamengine ila wee ni mwanamke @wema_memes naona furaha yako imetimia,” ameandika Esma kwenye Instagram, Jumatano hii.
Post hizo zinaonyesha kuwa familia ya Diamond hawapikiki kwenye chungu kimoja na Zari japo tayari ameshawazalia mtoto mmoja wa kike huku akitarajiwa kupata mtoto wa pili wa kiume miezi michache ijayo.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com